Tuesday, March 26, 2013

Gerrard na wenzake wameamua kufanya kweli


Gerrard, Lampard, Cole na Rooney wamekubaliana kufanya kweli kwenye michuano ya kombe dunia nchini Brazil mwaka 2014 wakianzia kwenye mechi za kufuzu. Gerrard amesema wamekubalina hivyo kwasababu wanaamini muda wao wa kuichezea timu ya taifa umefikia kikomo na kombe la dunia nchini Brazil ndiyo litakuwa la mwisho kwao wakiwa na timu ya taifa. Gerrard alisema toka wao waanze kucheza na timu ya taifa hawajawahi kushinda kikombe chochote hivyo huu ni muda wao wa mwisho na wamejipanga kucheza kufa na kupona ili waweze kuacha rekodi nzuri kwenye timu ya taifa. Gerrard alisema “mwaka jana tulijipanga kushinda Euro, tulifika mbali, lakini bahati haikuwa yetu, tulifanya makosa mechi yetu na Italy na kutolewa kwa penati 4-2”. England ilishinda kombe la dunia mwaka 1966 hadi sasa imepita miaka 47 na England haijawahi kuingia hata nusu fainali za kombe la dunia, kutokana na rekodi hizi Gerrard kama kepteni na wenzake wameamua kufanya kweli. England ipo kundi H ikiwa nafasi ya pili na pointi 11, leo inacheza na Montenegro ambao wanaongoza kwa pointi 13.

No comments:

Post a Comment