Hamilton leo amepatwa na aibu katika michuano ya Malaysian GP baada ya kujisahau na
kusimamisha gari lake kwenye gereji ya Mc Laren. Hamilton ambaye amejiunga na timu ya Mercedes hivi karibuni kutoka timu ya Mc Laren amesema nilijisahau kwasababu nimekuwa na Mc Laren kwa muda mrefu
sana, hivyo sikuweza kukumbuka mara moja. Mapema wiki hii Hamilton alisikika akisema anafurahia maisha yake ya sasa na ameshazoea mazingira yake mapya. Lakini usemi wake leo ulikuwa tofauti na kuonesha bado fikra zake zipo Mc Laren. DailyMail limeripoti.
No comments:
Post a Comment