Kiungo wa Man Utd Anderson amesema yupo tayari kurudi Porto
ili aweze kucheza kwenye fainali za kombe la dunia nchini kwao Brazil. Anderson
anayejisikia uchungu kuona hayupo kwenye kikosi cha taifa, ana mpango wa kuhama
Man utd ili apate timu atayoweza kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Anderson
anaamini kiwango cha kucheza timu ya taifa anacho ila hajaweza kumshawishi
kocha wa taifa kumuita kikosini kwasababu hadi sasa ameshacheza mechi sita tu
kwenye ligi na hana matumaini kama Sir Alex atamchezesha kwenye mechi zote
zilizobaki. Anderson ameitaja club ya Porto kuwa ndiyo timu anayofikiria kuwa
ataweza kurudi na kuonesha kiwango chake , habari hizi ni kwa mujibu wa
Footylatest.
No comments:
Post a Comment