Sunday, March 24, 2013

Taifa Stars 3 - 1 Morocco

Mbwana Samata
Timu ya Taifa ya Tanzania leo imeichapa timu ya Morocco katika michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Brazil 2014. Taifa Stars waliocheza mpira wa kuvutia imerudisha matumaini kwa Watanzania baada ya kuwa kichwa cha mwendawazimu kwa muda mrefu. Katika mchezo wa leo hadi mapumziko ilikuwa bila bila. Katika kipindi cha pili Stars ilianza mpira kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata magoli katika dk za 55, 74 na 87 wafungaji wa kiwa Thomas Ulimwengu (55) na Mbwana Samata (74,87)na Morroco walipata goli lao dk 90+. Kwa matokeo haya Taifa Stars imefikisha pointi sita na bado itaendelea kuwa nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast yenye point saba. Juni 7 mwaka huu Stars itakuwa ugenini kucheza mechi ya marudiano na Morocco. Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment