Wednesday, March 20, 2013

Kikosi Cha Morocco Kutua Nchini Ijumaa


Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.

No comments:

Post a Comment