Oscar Pistorius |
Nel wakili wa Pistorius akielezea jinsi tukio lilivyotokea alisema Pistorius alitembea mita saba kuelekea karibu na bafu, alipofika bafuni alimfyatulia risasi nne Reeva Steenkamp kupitia mlango ambao ulikuwa umefungwa. Kisha Pistorius alivunja mlango na kutoka nje akiwa ameubeba mwili wa mpenzi wake hadi chumba cha chini na alimuita rafiki yake mmoja akamweleza kuwa alidhani Steenkamp alikuwa mwizi ndiyo maana alifanya uamuzi wa kumuua. Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini bado anakabiliwa na wakati mgumu wa kujitetea mbele ya mahakama baada ya jaji wa kesi hiyo kusema kuwa mauaji hayo yalifanywa kwa kudhamiria na sio bahati mbaya.
No comments:
Post a Comment