Frank Lampard kiungo wa Chelsea anatarajia kukutana na kocha wa taifa la England Hodgson ili aweze kuongea naye kuhusu mipango yake kabla ya kufanya maamuzi ya kujaza mkataba mpya na Chelsea. Hodgson alisikika kwenye vyombo vya habari akisema anamshauri Lampard abaki England kama anapenda kuendelea kuwepo kwenye timu ya taifa. Hodgson aliyasema hayo baada ya vyombo vingi vya habari kuripoti kuwa Lampard ana nia ya kuhamia LA Galaxy ya Marekani. Uchunguzi umeonesha Lampard ameshaonesha nia ya kuhama Chelsea ila anapenda kuendelea kuwepo timu ya taifa ndiyo maana anahitaji kukutana na Hodgson ili waweze kukubaliana kabla ya kufanya uamuzi wa kuhama. Lampard anamaliza mkataba wake na Chelsea mwishoni mwa msimu huu na Chelsea imesema ipo tayari kusaini mkataba mpya na kiungo huyo ila Lampard mwenyewe amekuwa kigugumizi.
No comments:
Post a Comment