Kocha wa Real Madrid, Jose Mourihno amekanusha kuwa ana mpango wa kuhamia Man utd ndiyo maana alisema timu bora imefungwa baada ya kushinda goli 2-1 dhidi ya Man Utd. Mourinho alisema kauli yake hiyo ilikuwa na lengo la kuwapa nguvu wachezaji wake ili wajue bado wana kibarua kigumu hadi kufika fainali na kutwa ubingwa wa UEFA. "Kwasasa mimi nina mkataba na Real Madrid, naipenda timu yangu ya sasa, siwezi kuongea jambo ambalo sio jema kwa Real Madrid" alisikika Mourinho akisema hayo kwenye mahojiano na Real Madrid TV.
No comments:
Post a Comment