UEFA wamepunguza adhabu ya mshambuliaji wa PSG Ibrahimovic baada ya
kupata kadi mbili za njano katika mechi kati ya Valencia na PSG. Ibrahimovic
alikuwa amepewa adhabu ya kutocheza mechi mbili lakini UEFA imepunguza na
kubakiza mechi moja, mechi ambayo alishaadhibikia kati ya PSG na Valencia.
Kwahivyo Ibrahimovic atacheza mechi zote mbili kati ya PSG na Barcelona mwezi
ujao. Ibrahimovic ndiye mfungaji tegemezi wa PSG uwepo wake kwenye mechi muhimu
kama ya Barcelona ni nguvu tosha kwa PSG kufanikisha ushindi ikizingatiwa ni
mchezaji mrefu na mwenye nguvu ya kutetemesha mabeki wa Barcelona.
No comments:
Post a Comment