BBC inaripoti, Harambee Stars ya Kenya licha ya kupata mateso tangu wawasili nchini Nigeria kucheza na Super eagles katika mechi ya kutafuta kuingia katika kombe la dunia Jumamosi nusura wawaaibishe mabingwa wa Afrika kwa kutoka sare ya 1-1 huko mjini Calabar , Nigeria. Kenya ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia mchezaji Francis Kahata katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza. Licha ya Super Eagles kuwateremsha miamba yake yote kama vile John Obi Mikel na Victor Moses wa Timu ya Chalsea ya Uingereza lakini hawakufua dafu kwa kenya hadi mchezo unamalizika Kenya moja na Nigeria moja.
No comments:
Post a Comment