Sunday, March 24, 2013

Messi amkaribia Diego Maradona kwa magoli Argentina

Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, ameshafunga magoli 32 kwa timu yake ya taifa Argentina na kumkaribia Maradona mwenye magoli 34. Maradona ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi kuliko wote hadi sasa kwa timu ya taifa na pia ni mchezaji soka mfano kwa wengine nchini Argentina. Messi  ameonekana kuzifuata nyayo za Maradona toka alipoanza kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona, hadi sasa ameshacheza mechi 78 na timu ya taifa akiwa na magoli 32 wakati Diego Maradona alicheza mechi 91 na timu ya taifa na kufunga magoli 34.  Kwa mazingira ya kawaida Messi atampiku Maradona na atakuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kuliko wote nchini Argentina kwa timu ya taifa kwani amebakiza magoli mawili kumfikia Diego na bado umri wake unamruhusu kuendelea kucheza kwa miaka hata zaidi ya mitano. 

No comments:

Post a Comment