Boateng akisoma hotuba yake UN |
Kiungo wa Ac Milan Kevin Prince Boateng leo ametoa hotuba
yenye hisia kali kwenye kikao cha Umoja wa Mataifa (UN) katika kuadhimisha siku
ya kupinga na kutokomeza ubaguzi. Boateng alikwenda kutoa hotuba hiyo ikiwa ni
siku chache baada ya kufanyia kitendo cha kibaguzi na mashabiki wa timu ya Pro
Patria wakati Ac Milan ilipokuwa ikicheza mechi ya kirafiki. Katika tukio
hilo Boateng alitoka nje ya kiwanja kwa hasira na kukiomba chama cha soka nchi
Italia kuchukua hatua kwa kitendo hicho. Katika hotuba hiyo ambayo imewagusa
wengi, Boateng amesema “Ubaguzi ni kirusi hatari kisichokuwa na faida ambacho
kimeadhiri watu wengi. Katika kikao hicho Kevin aliongeza kwa kusema,
ataendelea kuwa balozi wa vita dhidi ya ubaguzi na atajitahidi akutane na Rais
wa FIFA Sepp Blatter ili aweze kumpatia mawazo ya kupigana na ubaguzi hasa kwenye
mchezo wa soka.
No comments:
Post a Comment