Thursday, March 21, 2013

Suarez hatoondoka Anfield


Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza Ian Ayre amethibitisha mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez ataendelea kuitumikia timu hiyo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 26 kutoka Uruguay,alinukuliwa siku za karibuni akisema atafikiria kuhusu kuihama Liverpool iwapo timu inayoshiriki michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Ulaya ingehitaji huduma yake,lakini Ian ameiambia BBC kuwa mchezaji huyo ataendelea kuvaa jezi nyekundu za majogoo wa Anfield msimu ujao. 

.

No comments:

Post a Comment