Sunday, March 24, 2013

Wenger ameopoa kifaa kipya Oboabona

Oboabona

Kocha wa Arsenal, Wenger ameopoa kifaa kipya Oboabona (22) kutoka Nigeria. Mchezaji huyo ameshashinda vikombe 18 akiwa Nigeria. Oboabona pia alikuwepo kwenye kikosi cha Nigeria kilichoshinda kombe la Mataifa ya Afrika nchini South Africa. Obo amekwenda England kwenye club ya Arsenal kwa majaribio na vipimo vya mwanzo vimeonesha kuwa Obo atabaki Arsenal. Obo mwenyewe amesema anaipenda Arsenal toka akiwa mdogo na yupo tayari kuichezea kwa moyo mmoja. Arsene Wenger ni kocha mwenye sifa kubwa duniani kwa kukuza vipaji na kuwainua wachezaji wadogo,  wakiwemo wengi kutoka Afrika kama Kolo, Adebayor na Alex Song. Obo akifanikiwa kwenye majaribio atanunuliwa kwa dola milioni 1. 

No comments:

Post a Comment