Arsene Wenger amesema atakuna na kocha wa England Hodgson ili kuongea naye kuhusu ratiba ya Wilshere kwenye timu ya taifa. Maamuzi haya ya Wenger yamekuja kwasababu England itakuwa na mechi mbili za kirafiki kati ya Ireland na Brazil mechi ambazo zitakuwa karibu na mechi za Arsenal. Kutokana na mazingira hayo Wenger amehitaji kuongea na Hodgson ili Wilshere apate kupumzishwa kwenye mechi hizo za England au kucheza dakaki chache ili aweze kucheza vyema kwenye mechi za Arsenal ambazo ni za muhimu zaidi katika kutafuta nafasi ya kushiriki ligi ya mabigwa ulaya.
No comments:
Post a Comment