Sunday, April 21, 2013

Djokovic ampiga Nadal Monte Carlo Masters

Bingwa mara nane mfululizo toka mwaka 2008 hadi 2012 Rafael Nadal leo ameutema ubingwa wake baada ya kupigwa kwa seti mbili mfululizo na Djokovic kwenye michuano ya tenesi ya Monte Carlo Masters nchini Ufaransa. Djokovic amempiga Nadal kwa seti 6-2, na 7-6 mchezo ambao ulikuwa mwepesi kwa Djokovic tofauti na mategemeo ya wengi. Nadal atasingizia kuwa ametoka kwenye kujiuguza majeraha kwa muda mrefu ndiyo maana amefungwa lakini ki-ukweli Djokovic yupo juu sana kwasasa na atagemewa kuendelea kushikilia nafasi ya kwanza duniani mwaka huu wote.  

No comments:

Post a Comment