Sunday, April 21, 2013

Goli la Luis Suarez dakika ya 95 laiduwaza Chelsea

Last laugh: Suarez denied Chelsea a win right at the death when he headed in Sturridge's cross
Goli la Luis Suarez lilifungwa dakika ya 95 ya mchezo limeongeza ushindani wa kuwania nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya Chelsea kutoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Liverpool. Kwa matokeo ya leo Chelsea wamebakia nafasi ya nne wakiwa na pointi 62 wakati Arsenal ipo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 63 na Tottenham nafasi ya tano pointi 61. Liverpool wenyewe wamefikisha pointi 51 wakiwa nafasi ya saba nyuma ya Everton yenye pointi 56. Magoli ya Chelsea yamefungwa na Oscar dk ya 26 na Hazard dk ya 57 (penati) na yale ya Liverpool yamefungwa na Sturridge dk 52 na Suarez dk ya 95.
Gesture: Benitez acknowledges the reception from the Liverpool faithful
Kocha wa Chelsea Rafa Benitez akiwapungia mkono mashabiki wa Liverpool walipokuwa wanamshangilia kwa furaha baada ya kuingia uwanjani leo wakati Chelsea ilipokutana na Liverpool. Benitez amepewa mapokezi hayo mazuri na mashabiki wa Liverpool ikiwa ni shukrani kwake akiwa kama kocha aliyeipa mafanikio makubwa Liverpool ikiwemo kombe la UEFA champions mwaka 2005.  

No comments:

Post a Comment