Saturday, April 20, 2013

John Terry agoma kumpa mkono Bosi wa FA

Beki mkongwe wa Chelsea John Terry jana alishangaza watu baada ya kugoma kumpa mkono mwenyekiti wa shirikisho la mpira la Uingereza bwana David Bernstein. Terry alifanya kitendo hicho kwenye siku ya makabidhiano ya kombe la UEFA kwenye ukumbi wa Banqueting jijini London. Terry na wachezaji wenzake wa Chelsea Lampard, Torres na Cech walikuwa wamepanga mstari kwa kusimama wakiwakaribisha wageni rasmi ambao ni waziri wa michezo wa England, raisi wa UEFA, meya wa London na mwenyekiti wa FA, wageni hawa kabla ya kukabidhiwa kombe na Chelsea walianza kwa kusalimiana ambapo mbele ya umati wote uliofurika kwenye ukumbi ukiongozwa na waziri wa michezo pamoja na raisi wa UEFA Michael Platini, John Terry aligoma kumpa mkono Bwana David Bernstein jambo ambalo lilimfanya Bernstein ajisikie aibu sana. Katika maelezo yake baada ya kutoka nje wa ukumbi John Terry alisema “nisingeweza kumpa mkono kwasababu kitendo alichonifanyia hakikuwa cha haki, yeye ndiye mbele kwenda mahakamani kuelezea kesi yangu na Anton Ferdinand”. Alipohojiwa bwana Bernstein kuhusiana na jambo hilo alisema “mimi siwezi kuongelea maswala ya kijinga, ila ni kweli mimi na Terry hatuna mahusiano mazuri tokea kesi yake itolewe hukumu”. John Terry mwaka jana alimfanyia kitendo cha kibaguzi mchezaji wa QPR Aston Ferdinand, kwa kitendo hicho alifungiwa kucheza mechi tano pamoja na kulipa faini ya paundi laki 220,000 jambo ambalo linamuuma John Terry hadi leo. 

Bernstein mwenyekiti wa FA akitabasamu kwa aibu huku akisalimiana na wachezaji wengine wa Chelsea baada ya kuchuniwa na John Terry aliyekuwa mbele ya mstari. 

No comments:

Post a Comment