Saturday, April 20, 2013

Man City yaongeza ofa kwa Cavani

Klabu ya Man City imetoa ofa kwa mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani ya paundi milioni 13.3 kama mshahara wake wa mwaka ili akubali kujiunga na klabu hiyo. Man City wametoa ofa hiyo ikiwa ni kubwa kuliko ya Real Madrid ili wamvutie Cavani kujiunga na Man City. Cavani akikubali ofa hiyo ya Man city basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi ya wote kwenye ligi ya Uingereza licha ya kuwa Cavani mwenyewe anapenda kwenda Real Madrid. Mbali ya Real Madrid na Man City, vilevile Chelsea, PSG na Man Utd wanamuwinda mshambuliaji huyu akiwa ni mbadala wa Falcao ambaye bado hajaonesha nia ya kuhama Atletico Madrid. Cavani  raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26 hadi sasa ameshacheza mechi 29 za ligi na anaongoza kwa ufungaji wa magoli katika ligi ya Italia akiwa na magoli 22. 

No comments:

Post a Comment