Uongozi wa klabu ya Yanga imegoma
mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu Tanzania bara na kuoneshwa kwa mechi zake na
kituo cha televisheni DSTV kupitia chaneli yake ya Supersport. Yanga katika
barua yake iliyopeleka kwenye uongozi wa TFF imesema haipo tayari kwa
mabadiliko hayo ya ratiba, kwani klabu imeshatumia gharama nyingi kuiandaa timu
na kusogezwa mbele kwa michezo ni kuwaongezea gharama za uendeshaji wa timu.
Pili klabu ya Yanga ilisikitishwa na Kamati ya Ligi na TFF kufikia makubaliano
na kituo hicho cha Luninga pasipo kuishirikisha timu ya Yanga ambao ndio haswa
walengwa wa mchezo huo, kwani mpaka sasa Yanga hawajui klabu itafaidika vipi na
matangazo hayo. Mbali ya Yanga kuandika barua hiyo lakini TFF na Kamati ya Ligi
bado hawajajibu barua hiyo mpaka sasa. Msimamo wa klabu ya Yanga ni kuwa
haitakubali kampuni ya DSTV kupitia kituo chake cha Supersport kuonyesha
michezo yake moja kwa moja bila ya kuongea na uongozi wa klabu ya Yanga. Hatua
hii ya Yanga imekuja baada ya TFF kupangua ratiba ya mechi sita ili ziweze
kuoneshwa moja kwa moja na kwenye luninga, kufuatia mabadiliko haya klabu
nyingi zimeonesha kutokukubaliana na TFF ikiwemo klabu ya Yanga
No comments:
Post a Comment