Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea jumamosi hii (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting. Ligi hiyo itaendelea jumapili (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi za wikiendi hii zinatabiriwa kutoa uamuzi wa ubingwa na mshindi wa pili kwani ikiwa Yanga na Simba zitashinda basi Yanga itakuwa imejihakikishia kuchukua ubingwa lakini ikiwa Simba itafungwa na Azam FC basi Azam FC itakuwa imejihakikishia nafasi ya pili na vilevile ikiendelea kugombani nafasi ya ubingwa pamoja na Yanga. Hivyo wapenzi wa mpira wa miguu nchini wanangojea dakika 90 za michezo hiyo ili kujua bingwa na wawakilisha wa nchi katika michuano ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment