Tanzania imependa kwa nafasi tatu
kwenye viwango vya FIFA duniani. Tanzania iliyokuwa nafasi ya 119 imepanda hadi
nafasi ya 116. FIFA imetoa matokeo hayo leo ambapo kupanda kwa Tanzania
kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na matokeo mazuri iliyoyapata kwenye mechi zake
iliyocheza mwaka huu na kushinda dhidi ya Morocco na Cameroon. Tanzania imeweza
kufikisha pointi 305 kutoka pointi 263 ilizokuwanazo awali. Kwa timu za Afrika,
Tanzania imepanda hadi nafasi ya 33 ikiwa juu ya Kenya ambayo ipo nafasi ya 34.
Kudhihirisha ubora wa Tanzania katika soka, Tanzania kwasasa ipo nafasi ya pili
kwenye kundi lake la kuwania kufuzu kombe la dunia ikiwa na pointi sita
tofauti ya pointi moja na vinara wa kundi hilo Ivory Coast wenye pointi saba, wakati timu ya Morocco inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi mbili na Gambia ni
ya mwisho ikiwa na pointi moja. Katika kundi hilo, Tanzania ipo mbele kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Morocco,
timu ambayo inashikilia nafasi ya 74 kwenye viwango vya FIFA ikiwa ni kiwango
cha juu mara mbili zaidi ya Tanzania, vilevile Tanzania imetofautiana pointi moja tu na
Ivory Coast, timu ambayo inashikilia nafasi ya 12 kwenye viwango vya FIFA duniani na nafasi ya kwanza kwa timu za Afrika. Kwa
kuonesha ushindani huu kwa timu ambazo zimeidizi viwango ni dhahiri kiwango cha
Tanzania kimekuwa kwa kiasi kikubwa sambamba na mchezo mzuri inayoonesha ikiwa
kiwanjani. Katika matokeo yaliyotoka leo timu ya Brazil imeshuka hadi nafasi ya
19 wakati Hispania ikiwa nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Ujerumani nafasi ya
pili na Ajentina nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment