Friday, May 10, 2013

Bale aongezewe mkataba na mshahara - Villa Boas

Kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas ameiomba klabu yake kuongeza mkataba na malipo ya Gareth Bale ili ajifunge zaidi kuitumikia klabu hiyo. Mkataba wa sasa wa Bale unakwisha mwaka 2016 na malipo yake ni paundi  75,000 kwa wiki, lakini Villas Boas amehitaji mchezaji huyo apewe mkataba wa miaka mitano na kuongezewa mshahara mara mbili zaidi ya sasa. Villas-Boas katika maongezi yake amesema anahitaji Bale afanyiwe hivyo kwasababu anacheza vizuri na kwa kiwango chake anastahili kulipwa kama wachezaji wengine wakubwa duniani na vilevile itamfanya aipende zaidi Tottenham na kumuondolea vishawishi vya kutaka kuhama kwenda kwenye vilabu vikubwa zaidi. Bareth Bale mwenye umri wa miaka 23 kwasasa anahitajiwa na vilabu vingi duniani ikiwemo Real Madrid, PSG na Man utd na dhamani yake kwasasa imeongezeka baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa Uingereza nakufikia paundi mil 80 – 100 akimpiku mshambuliaji wa Santos Neymar mwenye dhamani ya paundi mil 45-60. 

No comments:

Post a Comment