Saturday, May 11, 2013

Washabiki wa Simba, nia yetu ni kuondoa raha ya kushangilia ubingwa kwa Yanga tarehe 18

Mashabiki wa klabu ya Simba wamesema wanaimani na chipukizi wao kuwa watawafunga Yanga katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara utakaofanyika tarehe 18 mwezi Mei. Mashabiki hao wamesema wanauhakika na ushindi dhidi ya Yanga, kwani nia yao ni kuondoa utamu wa kutwaa kombe la ligi kwa vile wanajua siku ya tarehe 18 baada ya mechi ndipo Yanga atakabidhiwa kombe hivyo kama Yanga atafungwa na Simba kwenye huo mchezo basi raha ya kushangilia itakuwa imeingia dosari, lakini mchezaji wa zamani wa Simba Zamoyoni Mogella amesema chipukizi hao wa Simba wataweza kufanya maajabu hayo kama wataweza kutumia vyema kipindi cha kwanza ili wajipatie magoli ya kutosha mapema bila kuchelewa hadi kipindi cha pili ambapo huwa wanachoka na kuwapa mwanya wapinzani wao. Simba inayoshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwasasa imeamua kuwapa nafasi chipukizi wake kuonesha uwezo wao lakini vilevile kuwajenga ili waje kuchukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza, chipukizi hao wamekuwa wakicheza mechi kadhaa za mwisho wa ligi na wanatarajiwa kushuka dimbani tarehe 18 dhidi ya Yanga. 

No comments:

Post a Comment