Tuesday, May 28, 2013

Neymar kuvaa namba ngapi? 1 hadi 11 zina wenyewe

Neymar jerseys go on “sale.” Fans choose Thiago’s, Villa’s numbers
Kitandawili bado kipo kwa washabiki wa Barcelona kuhusu namba atakayovaa Neymar. Kutokana na kiwango cha Neymar washabiki wa Barca wanafirikilia kuwa ni lazima Neymar apewe namba ndogo (kuanzia namba 7 hadi 11) lakini mazingira yanaonesha namba 7 hadi 11 zote zina wenyewe (7- Villa, 8- Iniesta, 9-Alexis, 10-Messi na 11-Thiago). Ila ni wazi kwamba Iniesta na Messi namba zao haziwezi kuchukuliwa vilevile Alexis kwasababu ya ugeni wake ndani ya klabu. Lakini kwa upande wa Villa na Thiago inaonesha kati ya wachezaji hawa mmoja anaweza kuuzwa ili kutoa nafasi kwa Neymar kwani hadi sasa Thiago ameshatangaza nia yake ya kuhamia Man utd na Villa amehusishwa kwenda Arsenal au Tottenham, lakini kama wachezaji hawa wataendelea kuwepo Barca basi Neymar atalazimika kupewa namba nyingine ikwemo namba 20, 23 au 24.

No comments:

Post a Comment