Saturday, June 1, 2013

Bayern Munich kuweka historia nchini Ujerumani

Baada ya kushinda makombe mawili Uefa champions na kombe la ligi, klabu ya Bayern Munich leo itashuka dimbani kukutana na VFB Stuttgart katika fainali ya kutafuta bingwa wa kombe la shirikisho,mjini Berlin. Kama Bayern Munich watafanikiwa kushinda kombe hili, watakuwa wameweka rekodi nchini Ujerumani kwani hadi sasa hakuna klabu ambayo imewahi kushinda makombe matatu ya ligi, Uefa na shirikisho ndani ya msimu mmoja nchini humo. Mechi hii inatarajiwa kuchezwa saa tatu usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki.  

No comments:

Post a Comment