Saturday, June 1, 2013

Bayern Munich waweka rekodi nchini Ujerumani

Historic: Bayern Munich completed a famous treble with a 3-2 win over Stuttgart in the German Cup final
Klabu ya Bayern Munich imetwaa ubingwa wa kombe la shirikisho baada ya kuifunga klabu ya Stuttgart magoli 3-2. Hili limekuwa ni kombe la tatu kwa Bayern Munich msimu huu baada ya kushinda pia kombe la klabu bingwa ulaya (Uefa) pamoja na kombe la ligi kuu nchini Ujerumani. Ushindi huu unaifanya Bayern Munich kuweka historia ndani ya nchini hiyo kwani hakuna timu hata moja nchini Ujerumani ambayo imewahi kushinda makombe matatu ndani ya msimu mmoja. 
Ovation: Jupp Heynckes celebrates victory in Berlin before being lifted in the air by his Bayern team
Wachezaji wa Bayern Munich wakisherekea ushindi kwa kumrusha juu kocha wao Jupp Heynckes ambaye amemaliza muda wake leo hii wa kuifundisha klabu hiyo. Heynckes anaondoka huku akiwa ameacha rekodi ya kipekee ndani ya klabu hiyo jambo ambalo linamfanya Pep Guardiola ambaye anachukua nafasi yake kuwa na wakati mgumu wa kuendeleza mafanikio ambayo ameyaacha Heynckes. 

No comments:

Post a Comment