Saturday, June 8, 2013

Chelsea yawatema wachezaji nane

Malouda rarely featured this season for Chelsea (©GettyImages)
Katika kile kinachoitwa safisha safisha ya Jose Mourinho, klabu ya Chelsea imetangaza rasmi kuwatema wachezaji wake nane ambao wameonekana ni mizigo kwa klabu hiyo. Wachezaji hao ni Henrique Hilario, Ross Turnbull, Paulo Ferreira, Florent Malouda, Yossi Benayoun, Amin Affane, Archange Nkumu na Aziz Deen-Conteh. Mbali ya wachezaji hawa pia kuna wachezaji wengine wanatarajiwa kuuzwa ambao ni pamoja na David Luiz na Torres. David Luiz anatarajiwa kujiunga na Barcelona kama klabu hizi zitakubaliana kwani Barcelona wameshatuma maombi ya kumsajili Luiz na Torres anatarajia kutumika kama nyongeza ya pesa kwa kumsajili Cavani kutoka Napoli. 

No comments:

Post a Comment