Saturday, June 8, 2013

Higuain kwenye hatua za mwisho kwenda Arsenal

Higuain could be set for a move to Arsenal (©GettyImages)
Klabu ya Arsenal baada ya kutolewa nje na Man utd kumsajili Rooney sasa imehamia kwa mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuain. Taarifa zinasema kocha wa Arsenal, Arsene Wenger wiki hii amekutana na wakala pamoja na Baba mzazi wa Higuain nchini Ufaransa kuongelea uhamisho wa mchezaji huyo ili ajiunga na Arsenal. Haikujulikana maongezi hayo yafikia makubaliano yapi lakini alipoulizwa Higuain mwenyewe alisema “nimeshatangaza kuwa nitahama Real Madrid na Arsenal ni timu nzuri, naipenda na inanifaa sana kuendeleza soka langu kwasababu bado nina nguvu, na mambo yakiwa tayari kila kitu kitawekwa wazi”. Higuain alisema hayo alipokuwa akiongea na The Daily Mirror na tokea mchezaji huyo kutangaza kuwa atahama Madrid klabu ya Arsenal ndiyo imefikia hatua nzuri kumsajili mchezaji huyu. Wenger amepewa kiasi cha paundi mil 100 kwa ajili ya usajili na Higuain ameonekana kuwa ndani ya bajeti ya Arsenal kwani Madrid wametaka kiasi cha paundi mil 20 na mchezaji huyo anatarajiwa kulipwa paundi 130,000 kwa wiki.  

No comments:

Post a Comment