Tuesday, June 18, 2013

Ethiopia yapokonywa pointi 3 kufuzu kombe la dunia

Timu ya taifa ya Ethiopia imenyang'anywa pointi tatu na FIFA baada ya kumchezesha Manyahile Beyene kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia akiwa na kadi mbili za njano. Beyene alitakiwa asicheza mechi moja dhidi ya Botswana kutokana na kadi hiyo, lakini mchezaji huyo aliingia uwanjani, na matokeo yake timu ya Ethiopia, kocha mkuu pamoja na shirikisho la mpira nchini Ethiopia wameadhibiwa na FIFA sambamba na kupokonywa pointi tatu. Kutokana na kupokonywa pointi hizi Ethiopia kwasasa ina pointi 10 na imetolewa kwenye kundi la timu ambazo zimefuzu kuingia hatua ya mtoano. Licha ya kuwa na pointi 10 Ethiopia bado inaongoza kundi lake na itangojea hadi mechi yake ya mwisho dhidi ya Central African ili kujua kama itafanikiwa tena kufuzu kwa hatua ijayo. 

Msimamo wa Kundi la A ulivyo kwasasa
GROUP A
TeamMPWDLGFGAPts
Ethiopia54108310
South Africa5221848
Botswana5113584
Central African Republic51044103

No comments:

Post a Comment