Tuesday, June 18, 2013

Mechi za fainali FA cup kufanyika baada ya ligi

Job done: Ben Watson sealed Wigan's victory over Manchester City in last season's final
Kuanzia msimu ujao mechi za fainali za FA cup nchini Uingereza zitakuwa zinafanya wiki moja baada ya mechi za ligi kuisha. Uongozi wa FA umeamua hivyo ili kulipa heshima zaidi kombe hili kwani mechi ya fainali kufanyika baada ya ligi kuisha itatoa nafasi kwa watu wengi kufuatilia fainali za FA tofauti na mfumo uliokuwa ukitumika sasa ambapo fikra za wengi zilikuwa kwenye kombe la ligi. Kwa ratiba ya msimu ujao mechi ya fainali itafanyika tarehe 17 Mei siku sita baada ya ligi kuisha. 

No comments:

Post a Comment