Wednesday, June 5, 2013

Nadal vs Djokovic nusu fainali ya French Open

French Open
Bingwa namba moja duniani Novak Djokovic (Kushoto) na bingwa mara saba wa French open Rafael Nadal (kulia) watakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo kesho Juni 7 katika mchezo unaotarajiwa kuwa ni mkali na wakuvutia. Mshindi kati ya Djokovic na Nadal ndiye anayetarajiwa kushinda French open mwaka huu baada ya Federer kuondolewa ikizingatiwa kuwa nusu fainali ya pili inawakutanisha Tsonga na Ferrer ambao wanaonekana sio washindani wakubwa kwa Nadal na Djokovic. Nadal ameingia nusu fainali baada ya kumtoa Wawrinka kwa 6-2, 6-3, 6-1 na Djokovic alimtoa Haas kwa 6-3, 7-6, 7-5. Kwa upande wa wanawake nusu fainali itakuwa ni Serena vs Errani na Sharapova vs Azarenka. 

No comments:

Post a Comment