Friday, June 28, 2013

Casillas na Buffon wanamichezo wa kweli

Golikipa wa Hispania na Real Madrid Iker Casillas ameonesha kumkubali golikipa mwenzake wa Italia Buffon kwa kile kilichoelezwa na wachambuzi wa soka kuwa ndiyo uwanamichezo wa kweli. Mdadisi wa soka wa mtandao wa 101 na golikipa wa zamani wa Man utd, Peter Schmeichel wamesema, mwanamichezo yoyote wa kweli hasiti kuonesha mapenzi yake kwa mchezaji mwenye kiwango achokipenda. Schmeichel amesema kitendo cha Casillas kumfuata na kumkumbatia Buffon na kubadilishana naye jezi badala ya kwenda kushangilia ushindi na wenzake ni kitendo cha kishujaa na cha kuigwa kwa wanamichezo wengine. Casillas alifanya kitendo hicho jana usiku baada ya penati 7-6 kati ya Hispania na Italia kuisha, kama picha zinavyoonesha hapo chini

In pics: Spain, Brazil set up title clash
Picha hii inaonesha Casillas na Buffon wakikumbatiana wakati wachezaji wa Hispania wakionekana kwa mbali wakishangilia, ambapo kwa hali ya kawaida Casillas naye angekimbilia upande ambapo wachezaji wenzake wa Hispania walikimbilia kushangilia, lakini aliona ni vyema kumpa pole kwanza golikipa mwenzake kabla ya kushangilia. Casillas alifanya kitendo hiki kwa kile kinachosemwa ni kukubali kiwango cha Buffon akiwa ndiye golikipa anayemfagilia kuliko wote kwasasa.
Buffon y Casillas se abrazan tras el partido
Utani kabla ya penati kuanza 

Wakipeana salamu za mikono wakati wa penati

Angalia video Casillas na Buffon wakibadilishana jezi baada ya penati kuisha 

No comments:

Post a Comment