Saturday, July 6, 2013

Dwight Howard atua Houston Rockets

Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu timu gani atahamia Dwight Howard kwa misimu ijayo, taarifa rasmi zimeshatoka kuwa mchezaji huyu atahamia Houston Rockets. Taarifa hizi zimeua kabisa mipango ya timu za Dallas, Atlanta na Golden State ambazo zote zilikuwa zinahitaji kumsajili mchezaji huyu. Howard amesaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya dola mil 88. Taarifa hizi zimethibishwa na Howard mwenyewe kupitia akaunti yake ya Twitter akisema ‘nimeamua kuwa mchezaji wa Houston Rockets, nawashukuru wadau wote wa Los Angeles na nawatakia kila la heri’. 

No comments:

Post a Comment