Sunday, July 7, 2013

Neymar afanyiwa upasuaji ili kuongeza uzito

Ijumaa ya wiki hii mshambuliaji wa Brazil na Barcelona, Neymar alifanyiwa upasuaji wa koo ili kutoa tonsisi ambazo zilikuwa zinamsumbua kwenye upumuaji. Tatizo hili Neymar alikuwa nalo muda mrefu, ila mwenyewe hakuona lazima kumfanyiwa upasuaji. Lakini mwezi uliopita baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wa klabu ya Barcelona siku aliyosaini mkataba kuichezea klabu hiyo, Neymar aliambiwa na madaktari wa Barca kuwa uzito wake lazima uongezeke kwa kilo 5 ili aweze kuhimili mikiki ya ligi kuu na kombe la Ulaya. Madaktari wa Barca walitoa ushauri wa kutolewa tonsisi ili kumpa nafasi ya kupumua vyema jambo ambalo litamfanya aweze kuongezeka uzito. ‘Neymar ana kilo 64, ni kilo ndogo kulinganisha na Messi 77kg au Xavi 78 Kg. Lazima aongeza kilo 5 ili afikie kilo za wenzake, uzito wa kilo 5 zaidi utampa nguvu ya kupambana kwenye ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA champions). Tunashukuru upasuaji umefanyika salama, na ndani ya mwezi mmoja kilo zake zitaongezeka kabla ya msimu ujao haujaanza, na ataweza kucheza vyema zaidi ya sasa’. Hayo ni maneno ya daktari wa Barcelona, Ricard Pruna.

No comments:

Post a Comment