Thursday, August 1, 2013

Soldado atua Tottenham kwa paundi mil 26

Big money: Spurs will smash their transfer record with the signing of Roberto Soldado from Valencia
Klabu ya Tottenham imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Valencia na Hispania Roberto Soldado kwa paundi mil 26. Usajili huu wa Soldado umevunja rekodi ya usajili kwa klabu ya Tottenham kwani haijawahi kusajili mchezaji kwa gharama kubwa zaidi ya hii. Soldado anatarajia kufanyiwa vipimo na baadaye atasaini mkataba wa miaka mitano na atalipwa paundi 75,000 kwa wiki. Soldado anakuwa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa na Tottenham msimu huu baada ya Paulinho (Corinthians, £17m) na Nacer Chadli (FC Twente, £6m).

No comments:

Post a Comment