Wednesday, October 9, 2013

'Januzaj sio mtu sahihi kuchezea England' - Wilshere

Outspoken: Jack Wilshere believes only players born in England should be allowed to represent the country
Kiungo wa England na Arsenal, Jack Wilshere akiongea na waandishi wa habari jana jioni kuhusiana na mechi ya ijumaa kati ya England na Montenegro. Katika maongezi yake na waandishi, pia alimuongelea Adnan Januzaj. Wilshere alimuongelea Januzaj baada ya waandishi kumuuliza kama mchezaji huyu anapaswa kuichezea England. Wilshere alisema ' Wanaotakiwa kuchezea timu ya taifa ya England, wanatakiwa kuwa Waingereza, lazima wazaliwe ndani ya nchi hii. Sio sahihi mtu yoyote atakayeishi hapa kwa miaka mitano mfululizo basi aweze kucheza kwenye timu ya taifa. Hivyo kwa maoni yangu nahisi Januzaj sio mtu sahihi kuchezea timu ya taifa ya England'.

Wilmots is keen to have a meeting with Januzaj (©GettyImages)
Majadala wa nchi anayoweza kuchezea Januzaj bado ni tete kwani mchezaji huyu ana uhusiano wa nchi  tano, ambazo ni Albania, Serbia, Kosovo, Belgium na England. Hata yeye mwenyewe amesema bado hajajua ni nchi gani atachezea. 

No comments:

Post a Comment