Klabu ya Azam FC na kocha Stewart John Hall zimeamua kuvunja mkataba baina yao baada ya kuwa pamoja kwa kipindi kirefu cha mafanikio. Taarifa hizi zimetolewa leo kwenye matandao wa Azam FC, siku ambayo Azam Fc imetoka sare ya magoli 3-3 na Mbeya City. Katika taarifa yake, Azam wamesema kocha huyo na klabu wamekubaliana kwa pamoja kuvunja mkataba wao. Klabu ya Azam imemshukuru Stewart kwa jitihada zake katika kuijenga na kuifanikisha klabu ya Azam kwa moyo mmoja. Azam Fc hadi sasa inashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma ya Yanga. |
Thursday, November 7, 2013
Kocha wa Azam FC aachia ngazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment