Thursday, November 7, 2013

Messi na Ronaldo wakaribia rekodi ya Raul

CR
Messi na Ronaldo wamezidi kuikaribia rekodi ya Raul ya ufungaji wa magoli kwenye michuano ya Uefa champions. Hadi sasa Raul ana jumla ya magoli 71 wakati Messi 65 na Ronaldo 59. Ili kuifikia rekodi ya Raul, wachezaji hawa wawili (Messi na Ronaldo) itawabidi waendelee kufunga magoli kwa wingi, lakini uhalisia wa mambo unaonesha rekodi ya Raul itaweza kufikiwa msimu huu na Messi tu kwani amebakiza magoli sita kumfikia, lakini Ronaldo ataweza kumfikia Raul msimu ujao wa michuano hii kutokana na tofauti kubwa ya magoli iliyosalia.

Kumi ya wachezaji wenye jumla ya magoli mengi Uefa 

Raul 71
Lionel Messi 65
Cristiano Ronaldo 59
Ruud van Nistelrooy 56
Thierry Henry 50
Alfredo Di Stefano 49
Andriy Shevchenko 48
Eusebio 46
Filippo Inzaghi  46
Didier Drogba 42

No comments:

Post a Comment