Saturday, March 23, 2013

Iliniuma Ferdinand kujitoa timu ya taifa - Hodgson

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema alijisikia vibaya kuona Ferdinand akijiondoa kwenye timu ya taifa ya England baada ya kumuita kwaajili ya michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia dhidi ya visiwa vya San Marino na Mentengro.Hata hivyo kocha Hodgson akijibu swali kuhusiana na Ferdinand kusafiri hadi Qatar kuchambua mechi ambayo angekuwa uwanjani akicheza,alisema hakuwa na wazo lolote,lakini amejisikia vibaya kuona beki huyo hajajiunga na timu yake na kusafiri kwake kwenda Qatar licha yakuwa ni matakwa yake binafsi na klabu yake. Roy Hodgson amesema atasubiri kuona kama ataweza kumuita kwa mara nyingine beki wa Manchster United Rio Ferdinand.

No comments:

Post a Comment