Mdau Peter Chibanhila anaripoti kutoka uwanja wa taifa, kuwa timu ya Morocco imewasili muda sio mrefu kufanya mazoezi madogo madogo ikijiandaa na mechi ya Taifa Stars inayotarajia kufanyika kesho (tarehe 24) saa tisa mchana. Mechi ya kesho ni ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili. Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 3 baada ya kushinda mchezo mmoja na kushindwa mmoja. Kundi la Tanzania lina timu za Ivory Coast, Gambia na Morocco. Ivory coast wanaongoza wakiwa na pointi nne, wakati Morocco wakiwa wa tatu na pointi mbili, Gambia point moja nafasi ya nne. Picha ya chini kulia ni Mdau Peter akiwa mbele ya bango la kili stars.
No comments:
Post a Comment