Kocha wa Fc Barcelona Tito Vilanova
anatarajiwa kurejea wiki hii kutoka New York, Marekani alipokuwa anatibiwa
kansa. Tito amekuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili sasa na nafasi yake
imekishikiliwa na kocha msaidizi Jordi Roura. Tokea Tito aanze matibabu, Barcelona
haikupata matokeo mazuri ikiwemo kutolewa kwenye kombe la mfalme pamoja na
kufungwa mara kadhaa na mpinzani wao Real Madrid. Mtandao wa Barcelona uliongeza kuwa kurudi kwa Tito sio kwamba ataanza kazi mara moja, atachukua muda kidogo
kupumzika ila baadaye ataanza kazi. Barcelona kwasasa ina point 13 zaidi ya
Real Madrid kwenye ligi na April 2 itakuwa Ufaransa kucheza na PSG kwenye mechi ya UEFA.
No comments:
Post a Comment