Cristiano Ronaldo amesema atakwenda pamoja na wachezaji wenzake
wa timu ya taifa nchini Azerbaijan licha ya kuwa na adhabu ya kutocheza
kutokana na kadi mbili za njano. Ronaldo akiongea mbele ya
waandishi wa habari alisema “Nina kwenda kuipa support nchi yangu, nipo pamoja na
wenzangu kimwili na mawazo pia, hata kama sitocheza lakini uwepo wangu kwenye
benchi ni nguvu tosha kwa wenzangu nikiwa kama kepteni” Ronaldo alimalizia kwa
kusema "naamini mchango wangu nje ya uwanja utaaza matunda siku ya jumanne". Ureno ina pointi nane ikiwa nafasi ya tatu wakati Israel ipo nafasi ya pili na pointi nane ikizidiana magoli na Ureno na Russia nafasi
ya kwanza ikiwa na pointi 12.
No comments:
Post a Comment