Tiger Woods mcheza golf aliyekuwa nje ya 50 bora ya golf
duniani baada ya kukumbwa na matatizo ya kijamii kati yake na mkewe sasa
ameanza kurudi kwa kasi ya ajabu tofauti na ilivyofikiriwa na wapenzi wengi wa
golf kuwa hatoweza tena kufikia alipokuwepo. Tiger kwasasa anashikilia nafasi
ya pili chini ya Rory, na ataweza kupanda hadi nafasi ya kwanza kama atashinda Bay
Hill. Rory ana jumla ya point 529 wakati Woods ana jumla point 413 duniani.
No comments:
Post a Comment