Wachezaji wanne wa Azam FC
waliosimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi yao wameripoti
kambini tayari kuikabili Simba SC siku ya jumapili. Wachezaji hao ni Moradi,
Nyoni, Aggrey na Dida, kurejea kwa wachezaji hao kunamaliza mgogoro uliokuwepo
na Azam ambao ulidumu kwa takribani miezi mitano. Makubaliano hayo yamefikiwa
baada ya TAKUKURU kuchunguza tuhuma hizo na kuthibitisha kuwa wachezaji hao
hawaja husika na rushwa dhidi ya club ya Simba. Wachezaji hao wanatarajiwa
kuwemo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba SC ikiwa ni mchezo muhimu sana
kwa Azam FC kwani ikishinda itaizidi Simba SC pointi 14 huku Simba ikisaliwa na
michezo minne na hivyo kumaanisha kuwa Kagera Sugar atabaki kuwa mpinzani pekee
wa Azam FC katika kuwania nafasi ya pili.
No comments:
Post a Comment