Friday, April 19, 2013

Yanga wametoa sababu ya kutoka droo na Mgambo

Klabu ya Yanga baada ya kutoka droo ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Mgambo katika mechi iliyofanyika katikati ya wiki hii wamesema refa aliyechezesha mchezo huo hakuchezesha vizuri ndiyo maana wamepata matokeo mabaya na kusababisha kuumia kwa wachezaji wao. “Refa wa mchezo hakuwa ‘fair’ kabisa, alikuwa anawapendelea sana Mgambo, rafu nyingi alikuwa anaziachia kitu ambacho kimesababisha Yanga kupata majeruhi saba” hayo ni maneno yake Baraka Kiziguto msemaji wa klabu ya Yanga alipohojiwa akiwa Mabatini Kijitonyama kwenye mazoezi ya Yanga leo jioni. Wakati huo huo daktari wa Yanga amesema wachezaji sita kati ya hao walioumia siku ya mechi na Mgambo wanaendelea vizuri lakini Juma Abdul bado hali yake sio nzuri hivyo atahitaji muda zaidi ili aweza kupata nafuu. Yanga wapo kwenye maandalizi dhidi ya Ruvu JKT mchezo utakaofanyika jumapili ya April 21 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. 

No comments:

Post a Comment