Saturday, May 11, 2013

Lampard avunja rekodi ya Bobby Tambling

Frank Lampard
Frank Lampard apiga goli la 202 na 203 na kumzidi Bobby Tambling ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kuliko wote kwenye historia ya Chelsea. Tambling alihama Chelsea mwaka 1970 akiwa na magoli 202, tokea mwaka huo hadi leo hakuna mchezaji aliyeweza kuifikia rekodi yake kabla ya Lampard kuivunja leo. Lampard ameweza kufunga magoli hayo leo katika mechi dhidi ya Aston Villa na kuifanya Chelsea kutoka na ushindi wa goli 2-1. Lakini kuna utofauti wa mechi kati yao, kwani hadi Tambling anaondoka Chelsea alikuwa ameshacheza mechi 302 lakini Lampard ameweza kufikisha magoli hayo kwasababu ameshacheza mechi 402 ikiwa ni mechi 100 zaidi ya Tambling. 

No comments:

Post a Comment