Friday, May 31, 2013

Mutu atangaza nia ya kumlea mtoto aliyeokotwa kwenye bomba la maji machafu nchini China

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu ameomba mamlaka za nchini China zimruhusu kumchukua mtoto aliyeokotwa kwenye bomba la maji machafu ili amlee. Mtoto huyo aliyezaliwa na uzito wa kilo 2.5 alikutwa ametupwa ndani ya bomba la maji machafu lenye ukubwa wa sentimita 10 na aliweza kuokolewa kwa msaada wa kikosi cha zimamoto wakishirikiana na madaktari. Tukio hili lilitangazwa sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na kugusa hisia za watu wengi, tukio ambalo lilimgusa pia Mutu na kutoa uamuzi wake wa kumuomba mtoto huyo. Mutu alisema " baada ya kuona taarifa hiyo nilishikwa na hisia zilizonituma kumsaidia mtoto huyu na nilimwambia mke wangu Consuelo tukakubaliana tumchukue, ila inabidi tufuate taratibu ili kuweza kumchukua".  
Mtoto akitolewa ndani ya bomba baada ya kukatwa na kikosi cha zimamoto 
Mtoto akiwa hospitali hivi sasa na imeripotiwa kuwa anaendelea vizuri akiwa chini ya uangalizi wa madaktari maalumu nchini China. 

No comments:

Post a Comment