Saturday, June 1, 2013

Juma Kaseja haondoki Simba - Hans Poppe

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Simba Hans Pope amethibitisha kuwa golikipa wa klabu hiyo Juma Kaseja hatoondoka msimu huu. Pope aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mipngo ya klabu ya Simba kuhusu usajili wa wachezaji kwa msimu ujao. Pope aliongelea swala la Kaseja kutokana na tetesi zilizopo kuwa anatarajiwa kuondoka ndiyo maana klabu hiyo imeamua kusajili golikipa mwingine. Hans Pope alijibu jambo hili kwa kusema "Kaseja ni golikipa wa siku nyingi, anajiheshimu sana, kama angekuwa anataka kuhama angesema muda mrefu kwani ni kawaida yake, nakumbuka mwaka aliokwenda Yanga alikuja kutujulisha mapema na sisi tulimruhusu, kwasababu sera zetu haziruhusu kumkataza mchezaji kuondoka kama anataka, kwahivyo Kaseja bado ni mchezaji wetu na tutaendelea kuwa naye msimu ujao na suala la kusajili kipa mpya ni mipango tu ya klabu katika kuimarisha timu". Vilevile Pope aliongea swala la kiwango cha Kaseja, ambapo baadhi ya wadau wa soka wamedai kuwa kiwango chake kimeshuka, Pope alisema "inawezekana kuwa kiwango cha Kaseja kimeshuka, ukilinganisha na miaka ya nyuma lakini hadi sasa hakuna golikipa anayefikia kiwango chake ndiyo maana bado ni golikipa tegemezi wa timu ya taifa.  

No comments:

Post a Comment