Saturday, June 1, 2013

Taifa stars inaweza kuondolea kwenye michuano ya kombe la dunia - Kayuni

Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni amesema timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ipo kwenye hatihati ya kutolewa kushiriki kwenye michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia kufuatia mdau mmoja wa soka kufungua kesi katika mahakama ya Kibaha akilishtaki shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kuiondoa timu ya Kiluvya katika michuano ya ligi ya mabingwa wa mikoa. Kayuni aliongea hayo alipokuwa akiongea na ITV na amemuomba mdau huyo kuiondoa kesi hiyo mara moja mahakamani kwani Taifa stars kwasasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo, hivyo kitendo hicho kinaweza kuifungia Tanzania na timu ya taifa kupoteza mafanikio yake yote iliyoyapata hadi sasa. TFF imetoa ombi hili kwani sheria za soka zinazosimamiwa na FIFA haziruhusu maswala ya soka kuamuliwa na mahakama au kuingiliwa na serikali hivyo  kitendo hichi kinaweza kusababisha Tanzania kufungiwa na FIFA kushiriki kwenye michuano yoyote iliyopo  chini ya FIFA. Ifuatayo ni taarifa ya Sunday Kayuni kama inavyoripotiwa na ITV

No comments:

Post a Comment